BAADA YA KUKOSA UBUNGE AZUNGUMZIA KUZIKWA. - Rhevan Media

BAADA YA KUKOSA UBUNGE AZUNGUMZIA KUZIKWA.


Afande Selle alisema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio na kusisitiza kuwa siku atakayo kufa anaomba achomwe moto kwani yeye anaamini katika moto na si kuzikwa kawaida.

Afande Sele alidai kuwa amechoka kuwa binadamu bali anataka kuwa Malaika ndio maana anahitaji kuchomwa moto ili siku ya ufufuo arudi kama Malaika na si binadamu, imani yake inamtuma kuwa akizikwa kwenye udongo siku ya ufufuo atarudi kuwa binadamu tena jambo ambalo yeye hataki kulisikia tena.

Kufuatia imani hiyo Afande Sele amesema mpaka sasa ameacha wosia kuwa siku atakayokufa achomwe moto na si kuzikwa.
Previous
Next Post »