WALIMU MARUFUKU KUPAKA WANJA - Rhevan Media

WALIMU MARUFUKU KUPAKA WANJA

Serikali wilayani hapa Mkoa wa Geita, imepiga marufuku walimu kuvaa mavazi yasiyolingana na taaluma yao na upakaji wanja na rangi ya mdomo kupita kiasi wanapokuwa kazini.
Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Geita, Thabitha Bugema alitoa amri hiyo leo wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za msingi na waratibu elimu kwenye kikao cha muongozo wa kutumia fedha za elimu bure zilizotolewa na Serikali
Previous
Next Post »