KIBATALA AANDIKA WARAKA MZITO KWA TUNDU LISSU - Rhevan Media

KIBATALA AANDIKA WARAKA MZITO KWA TUNDU LISSU

Wakili wa kujitegemea, Peter Kibatala ameandika waraka kwa Rais wa chama cha Wanasheria wa Tanganyika  (TLS) ,Tundu Lissu kwamba atahakikisha anatumia ujuzi wake wote wa sheria kuhakikisha katazo la IGP Sirro kuhusu mjadala wa kiongozi huyo kupigwa risasi linatenguliwa.

Kibatala ameweka waraka wake kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa yamepita masaa machache baada ya IGP Sirro kutoa kauli ya katazo kwa wanasiasa kuhusu kuuendeleza mjadala wa Lissu na kuwataka waliachie jeshi la polisi liendelee kufanya kazi yake.

Kibatala ameandika "Mpendwa Kaka Tundu Lissu wanasema eti wamekataza mjadala juu ya wewe kupigwa risasi 11 mwilini mwako, kati ya zile 38 zilizoelekezwa kwako.binafsi nitatumia ujuzi wangu wote wa kisheria kuhakikisha hilo katazo linatenguliwa. Ile tu kupambana kuhakikisha hicho kitu hakina mashiko kisheria ni sehemu ya kutimiza wajibu wangu kwako .

Waraka ukaelezea zaidi; "U are my President, now and forever, my whole some President na i will be very stupid to leave such legal issues un-attended". (Nitakuwa mpumbavu nikiiacha ishu hii ya kisheria bila kuishughulikia Rais wangu, Wewe ni rais wangu sana na hata milele".

Hata hivyo katika waraka wake huo Kibatala ameomba radhi kwa Rais wake huyo kwa kutowekeza nguvu zake kwenye sintofahamu za Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa Ben Saanane aliyepotea kusikojulikana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa Alphonce Mawazo aliyeuawa na watu wasiojulikana, huku akimuahidi kuanza kutafuta ufumbuzi wa kisheria kwenye masuala hayo.

"Nisamehe sikuwekeza nguvu za kisheria za kutosha kwenye issues za Ben Saanane na Alphonce Mawazo. Mimi na wenzangu tutatumia kila mbinu ya kisheria kuhakikisha mambo haya yanapatiwa ufumbuzi wa umma kwa sababu upelelezi kisheria si mali binafsi ya jeshi lolote nchini" Kibatala ameongeza.

Kibatala ameongeza "Tundu Lissu ukirudi utanikuta nipo njiani na masuala haya na kwa vyovyote wewe  au mwingine 'who will be left standing or sitting, will carry through' .

Hata hivyo mwisho wa waraka huo Kibatala amesema  ajenda yake kuu wiki hii itakuwa pia ni kuuliza kisheria uhalali wa kuzuia maombi ya wazi kwako Tundu Lissu.

Previous
Next Post »