RAIA WA BURUDI '' WALIOTAKA KUJIUNGA NA AL-SHABAB '' WAKAMATWA - Rhevan Media

RAIA WA BURUDI '' WALIOTAKA KUJIUNGA NA AL-SHABAB '' WAKAMATWA


Tokeo la picha la AL SHABAB

mage captionWapiganaji wa al-Shabab nchini Somalia
Police nchini Kenya wamewakamata watu wanne wanaoaminika kuwa raia wa Burundi ambao walikuwa wakielekea Somalia kujiunga na kundi la al-Shabab.
Maafisa wa ujasusi walikuwa wakiwafuata washukiwa hao baada ya kupata habari kuhusu mipango yao, kulingana na msemaji wa polisi George Kinoti.
Ameongezea kwamba washukiwa wanne walikamatwa katika kizuizi cha polisi mjini Isiolo takriban kilomita 350 kaskazini mwa mji mkuu wa nairobi wakielekea katika mji wa mpakani wa Mandera.
Maafisa wa polisi pia wanasema wanne hao waliingia nchini Kenya kama watalii kupitia visa huru ya ushirikiano kati ya Burundi na Kenya.
Maafisa katika Ubalozi wa Burundi mjini Nairoibi wanasema kuwa watatoa taarifa kamili kuhusu kukamatwa huko baada ya kushauriana na mamlaka ya Kenya.
Mnamo mwezi Januari mwaka huu raia mwengine wa kigeni, ambaye alikuwa Mtanzania alikamatwa mjini Mandera akijaribu kuvuka na kuingia Somalia kwa lengo la kujiunga na kundi hilo la al-Shabab.
Previous
Next Post »