MDOGO WA TUNDU LISSU AFUNGUKA MAZITO SAKATA LA KAKA YAKE KUPINGWA RISASI - Rhevan Media

MDOGO WA TUNDU LISSU AFUNGUKA MAZITO SAKATA LA KAKA YAKE KUPINGWA RISASI


Mdogo wake na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anayefahamika kwa jina la Vicent Lissu Mughwai amefunguka kuhusu sakata la kaka yake kupigwa risasi na kusema anaumia kwa ajili ya Watanzania.

Mdogo wake na Tundu Lissu amesema hayo jana alipokuwa kwenye kanisa la Ufufuo na uzima ambao aliwashukuru Watanzania kwa kumuombea kaka yake huyo ambaye kwa sasa anaendelea vizuri na kudai kuwa anaamini kupitia yeye haki ya nchi itapatikana kwani ili haki ipatikane lazima watu wengine waumie.

"Mimi ni mdogo wake na Tundu Lissu akitoka yeye kuzaliwa ndiyo mimi nafuata, baba askofu naanza kukushukuru kwa maombezi maalum kwa ajili ya ndugu yangu huyu lakini pia nawashukuru Watanzania wote kwa maombezi ndugu zangu nimekuja hapa kusema kitu kimoja tu ni shukrani kwa sala zenu, tuko hapa leo ndugu yangu Lissu amelala hospitalini alipigwa risasi nyingi sana, nilibahatika kwenda siku hiyo hiyo, tulikwenda moja kwa moja hospitalini Dodoma, madaktari wengi walifanya kazi nzuri sana, wataalamu wanasema katika matukio kama hayo yale masaa ya mwanzo ni "very critical" alipigwa risasi nyingi sana na kuvuja damu nyingi"  alisisitiza mdogo wake Tundu Lissu

Mdogo wake na Tundu Lissu aliendelea kusema kuwa "Tukio hili lilitokea kwenye sehemu ambayo ni sehemu ya mawaziri, mimi namjua Lissu ni mtu ambaye anapenda haki sana, toka utotoni, kinachoumiza zaidi mtu ambaye anataka haki, mtu anayetaka usawa kwa watu wote, mtu anayepigania haki za katiba leo yupo kitandani na ilikuwa awe amekufa lakini kwa nguvu za Mungu aliyehai Lissu leo yupo mzima na tunaomba na kushukuru na tunaomba tuendelee kumuombea ndugu yetu" alisema mdogo wake na Tundu Lissu

Aidha Mdogo wake na Tundu Lissu amesema kuwa anashangaa kwanini vyombo vya usalama havikutaka kufanyia kazi taarifa ambayo awali alishaitoa kuhusu watu ambao wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu ambao alishawahi kuwasema katika mkutano wake na vyombo vya habari.

"Bahati mbaya sana watu wanaotetea haki ndiyo wamekuwa wakiumia, ndugu yangu karibu miezi miwili hivi alikuwa anafuatwa na watu na alitoa taarifa tena aliongea na vyombo vya habari kuwa nafuatwa kila napokwenda, lakini ndiyo hivyo tena ila tunaimani kwa nguvu ya Mungu atapona, naomba nitumie nafasi hii kuwaomba tuendelee kuzidi kumuombe, naamini nchi yetu itakuwa na amani na haki kwani muda mwingine haki inapatikana baada ya watu wengine kuumia kama ambavyo ndugu yangu ameumia" alimaliza mdogo wake na Tundu Lissu

Previous
Next Post »