Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini kwa kurusha kombora kupitia anga la japan, huku nchi hiyo ikithibitisha kutekeleza.
Taarifa iliyoandikwa na Marekani, haikutishia kuiwekea vikwazo vipya Korea kaskazini.
Lakini Baraza la Usalama limeitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio zaidi na kusitisha mpango wake wa nuklia.
- Baraza la Usalama la UN lailaani Korea Kaskazini
- UN yatishia kuichukulia hatua Korea Kaskazini
- Korea Kaskazini yawaachilia raia wa Malaysia
- Korea Kaskazini kutengeza kombora la masafa marefu
Wanachama 15 wa Baraza hilo la Usalama wameitaka korea kaskazini kuchukua hatua za haraka kupunguza hali ya wasiwasi uliyopo.
Majeshi ya Korea kusini na Marekani yamekuwa yakifanya mazoezi ya pamoja karibu na mpaka wa Korea kaskazini, jambo ambalo Pyongyang inasema ni mazoezi yenye kulenga uvamizi wa kijeshi.
Sign up here with your email

