VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI WANAOJIUZURU MKOANI ARUSHA WAELEZA SABABU - Rhevan Media

VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI WANAOJIUZURU MKOANI ARUSHA WAELEZA SABABU

Tokeo la picha la BENDERA YA CHAMA CUF
Viongozi wa vyama vya Upinzani wanaoendelea kujiuzulu mkoani Arusha wamesema wanalazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kunyimwa fursa ya KUSHIRIKIANA na Viongozi na watendaji wa SERIKALI KUTATUA KERO za wananchi.

MMOJA wa viongozi hao Bw. Edward Moita ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Moita wilayani Monduli kwa Tiketi ya Chadema amesema inakuwa vigumu kufanyakazi kwa utaratibu uliopo sasa hivi ambao kila anayeshirikiana na watendaji wa serikali anaonekana msaliti. 
Alisema kimsingi anachokijua yeye ni kwamba pamoja na kuwa kiongozi kwenye chama cha Upinzani anapaswa kushirikiana na watendaji walioko madarakani kutatua kero za wananchi lakini baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakiona kama ni usaliti. 
Baadhi ya wananchi wakiwemo wa Kata hiyo wamesema wametofautiana mitazamo juu ya kujiuzulu kwa madiwani hao ambapo baadhi yao wamefurahia na wengine wamesema wanachotaka ni kuona matatizo yao yanapata ufumbuzi na wanakuwa na maendeleo. 
Kabla ya kujiuzulu Diwani huyo wa kata ya Moita Edward Moita ambaye ni wa kwanza kujiuzulu katika wilaya ya monduli lakini akiwa ni wa saba katika mkoa wa Arusha amewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli na pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika uongozi wa mila wa jamii hiyo.
Previous
Next Post »