TAASISI YA TWAWEZA KUPITIA SAUTI ZA WANANCHI LEO INATOA RIPOTI HII HAPA NYETI - Rhevan Media

TAASISI YA TWAWEZA KUPITIA SAUTI ZA WANANCHI LEO INATOA RIPOTI HII HAPA NYETI

Tokeo la picha la TWAWEZATaasisi ya TWAWEZA kupitia Sauti za Wananchi leo inatoa ripoti ya maoni ya Wananchi kuhusu Usalama, Polisi na Haki nchini.

Kumekuwepo na mfululizo wa matukio ya mauaji yanayotishia hali ya Usalama nchini hususani yake yanayotokea Kibiti, Mkoani Pwani. .

Ripoti hii itatoa mtazamo wa Wananchi kuhusu hali ya usalama. Baadhi ya maswali yatakayojibiwa ni:- .

Ni kwa kiasi gani wananchi wanajisikia wapo salama kwenye nyumba zao na katika maeneo wanayoishi?

Wananchi wana uzoefu gani kuhusu uhalifu?

Jeshi la polisi lina jukumu gani katika kuhakikisha ulinzi na usalama?

Viongozi wa serikali za mitaa na sungusungu wana jukumu gani?

Ni kwa kiwango gani wananchi wana imani na uwezo wa mifumo ya utoaji haki katika kuwaadhibu wananchi na watu maarufu wanaofanya uhalifu?
Previous
Next Post »