HAKUNA MSWALIE MTUME ... VITUO VYA MAFUTA KUENDELEA KUFUGWA KISA HIKI HAPA - Rhevan Media

HAKUNA MSWALIE MTUME ... VITUO VYA MAFUTA KUENDELEA KUFUGWA KISA HIKI HAPA

Vituo kadhaa vya kuuza  dizeli, petroli na mafuta ya taa vimefungwa jijini hapa kutokana na kutokuwa na mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs).

Hatua hiyo inayotekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeelezwa kuwaathiri si tu wenye vituo bali hata watumiaji.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema leo  Julai 14 na kuongeza kwamba  wanaendelea na kazi hiyo nchi nzima ili kuhakikisha sheria inatekelezwa.
Previous
Next Post »