Mahakama ya Misri imependekeza adhabu ya kifo kwa watu thelathini waliotiwa hatiani kwa kuhusika kwenye mauaji ya mwendesha mashtaka mkuu wa nchi hiyo.
Hisham Barakat alikufa kwenye shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari miaka miwili iliyopita.
Alikuwa miongoni mwa maafisa waandamizi wakuu kuuawa na wanamgambo katika miaka ya karibuni.
Bwana Barakati alihusishwa na maelfu ya kesi ya wapiganaji wa Kiislamu kufuatia mapinduzi ya serikali ya Misri iliyokuwa ikiongozwa na Muslim Brotherhood.
Mamlaka za dini za nchi hiyo sasa wataamua iwapo waidhinishe hukumu ya vifo iliyopitishwa na mahakama.
Misri iliwalaumu kundi la Musclim Brotherhood na lile la Gaza la Hamas kwa mauaji ya Bwana Barakat licha ya makundi yote mawili kukana kuhusika
Mwaka uliopita wizara ya mambo ya ndani ilitoa video ikionyesha wanaume kadha wakikiri kuhusika kwenye mauaji hayo na kusema kuwa walienda huko Gaza kupata mafunzo kutoka kundi la Hamas.
Baadaye baadhi yao walikana madai hayo mahakamani wakisema kuwa walikuwa wameteswa ili kukiri.
Sign up here with your email