Watu waliokuwa na silaha wamefyatua risasi katika bunge la Iran na katika madhabahu ya Ayatollah Khomeini katika mji mkuu Tehran .
Sauti kali za risasi zilisikika kutoka ndani ya bunge na kuna ripoti kuwa mlizji mmoja aliuawa.
Watu kadha walijeruhiwa katika kaburi la mwanzilishi wa taifa la kisasa la Jamhuri ya Iran.
Kulikuwaa na mlipuaji wa kujitoa mhanga na watu wengine wawili au watatu waliokuwa na bunduki.
Vikosi vya usalama vimefurika nje na ndani ya jengo la bunge.
Ripoti za hivi punde zinasema kuwa shambulizi katika bunge la Uingereza bado linaendelea
Shirika la habari la Iran IRIB lilimnukuu mbunge mmoja akisema kuwa kulikuwa na washambualiaji kadha katika majengo ya bunge waliokuwa wamejihami na bunduki aina ya AK-47.
Shirika hilo la habai lilisema kuwa walinzi wawili walijeruhiwa.
Ripoti zinasema kuwa ufyatuaji risasi katika kaburi la Ayatollah Khomeini ulifanyika wakati mmoja.
Sign up here with your email