RAIS MAGUFULI AWAPA WANANCHI ARDHI EKARI 65 ZA MAGEREZA - Rhevan Media

RAIS MAGUFULI AWAPA WANANCHI ARDHI EKARI 65 ZA MAGEREZA

Tokeo la picha la SHAMBA LA MAGEREZA

Pwani. Rais John Magufuli amewapa wakazi wa Bagamoyo, eneo la Magereza lenye ukubwa wa heka 65.
 Rais Magufuli amechukua uamuzi huo leo (Alhamisi) wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.
Alichukua hatua hiyo baada ya wanawake waliokuwa wamebeba mabango, kumtaka awape eneo lao kwa kuwa ni wazaliwa wa Bagamoyo, ni wajane na wana uhaba wa maeneo ya biashara.
“Akina mama mnaokaa huko na akina baba nimewapa hilo eneo lakini natoa tahadhari, mpaka wenu sasa ni barabara, msivuke mkaenda upande ule,” amesema.
Amelitaka Jeshi la Magereza kufanya mabadiliko katika hati ili eneo hilo liwe la wananchi.








Previous
Next Post »