MWANAMFALME HARRY : HAKUNA ANAYETAKA KUWA MFALME UINGEREZA - Rhevan Media

MWANAMFALME HARRY : HAKUNA ANAYETAKA KUWA MFALME UINGEREZA

Mwamfalme Harry
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwamfalme Harry
Hakuna mtu hata mmoja katika familia ya ufalme wa Uingereza anayetaka kuwa malkia ama hata mfalme ,mwanamfalme Harry ameliambia jarida moja la Marekani akiongezea kuwa wao huwajibika kulingana na muda.
Je kuna mmoja yenu ambaye anawania kuwa mfalme ama hata malkia?
Sidhani, aliambia jarida la Newsweek.
Aliongezea kuwa familia hiyo ya ufalme inawajibika kuwatendea wema raia wa Uingereza.
Mwanamfalme Harry pia alizungumza kuhusu msafara wa mazishi ya mamake Diana akisema haifai kwa mtoto wa miaka 12 kushiriki.
Mwanamfalme William na Harry wakati wa mazishi ya mama yao
Image captionMwanamfalme William na Harry wakati wa mazishi ya mama yao
Mwaka 1997 Harry alijiunga na babake ,mwanamfalme wa Wales, babuye na mjombake Earl Spencer katika msafara wa barabara za mji wa London.
Harry ambaye hivi majuzi alisema amepokea ushauri ili kuweza kuhimili kifo cha mamake katika ajali mjini Paris, alisema: Mamangu alikuwa amefariki na nikalazimika kutembea kwa muda mrefu nyuma ya jeneza lake, tukiwa tumezungukwa na maelfu ya watu wakiniangalia huku mamilioni wengine wakiangalia kupitia runinga.
Sidhani kama mtoto anafaa kuambiwa afanye hivyo, kwa udi na uvumba, sidhani kama itafanyika hii leo.
Previous
Next Post »