MD KAYOMBO: MIL 85,000,000 ZAPATIKANA ZITAJENGA MADARASA MATANO SHULE YA MSINGI HONDOGO - Rhevan Media

MD KAYOMBO: MIL 85,000,000 ZAPATIKANA ZITAJENGA MADARASA MATANO SHULE YA MSINGI HONDOGO

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 14,
2017 Ameeleza dhamira yake kuhusu ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa
katika shule ya Msingi Hondogo iliyopo katika Kata ya Kibamba.
MD
Kayombo ametoa ufafanuzi huo ofisini kwake alipokuwa akitoa tathmini ya
ziara yake aliyoifanya katika Shule ya Msingi Hondogo Jana tarehe 13
June 2017.
Katika ziara hiyo
ambayo Mkurugenzi aliambatana na Mchumi Mkuu wa Manispaa, na Ofisa Elimu
Msingi walikagua maeneo yote ya shule hiyo ikiwemo majengo na kubaini
kuwa Kuna baadhi ya majengo ambayo yapo katika hali ya uchakavu hivyo
kuamua kujenga madarasa mapya matano ili kuwaimarishia wanafunzi kuwa na
mazingira rafiki ya kusomea.
Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa
ujenzi huo utakaoanza hivi karibuni wa vyumba vitano vya madarasa
unaakisi pia ujenzi wa vyumba vya madarasa nane na matundu ya vyoo
katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, vivyo hivyo katika Shule ya Msingi
Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza
kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi
na walimu.
Mkurugenzi Kayombo ameishukuru Bank ya CRDB kwa
kuchangia shilingi Milioni 68,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa
hayo ambapo ameeleza kuwa Ofisi yake imetoa jumla ya shilingi milioni
17,000,000.

Previous
Next Post »