MAREKANI YAENDELEZA UBABE SYRIA , YAITUNGUA NDEGE NYINGINE - Rhevan Media

MAREKANI YAENDELEZA UBABE SYRIA , YAITUNGUA NDEGE NYINGINE

Marekani imeendeleza ubabe wake wa kuzitungua ndege za kijeshi za Syria mara baada ya kuitungua ndege nyingine isiyo na Rubani kusini mwa nchi hiyo.

Marekani inadai kuwa ndege hiyo iliyotunguliwa ya Jeshi la Syria ilikuwa imebeba silaha nzito na hatari kwa Jeshi la Marekani la ardhini hivyo imechukua hatua hiyo kwaajili ya kujikinga na hatari ya kushambuliwa.

Hiki ni kisa cha karibuni kabisa katika anga ya Syria, baada ya Marekani kuangusha ndege ya kivita ya Syria siku ya Jumapili na ndege nyingine isiyo na rubani mapema mwezi huu.

Katika taarifa nyingine jeshi la Marekani lilitangaza rasmi kuwa lilimuua kiongozi wa cheo cha juu wa kundi la Islamic State Turki al-Binali, wakati wa shambulizi lililofanywa na ndege nchini Syria Mwezi uliopita.
Previous
Next Post »