KITAMBI AISUBIRI KWA HAMU YANGA - Rhevan Media

KITAMBI AISUBIRI KWA HAMU YANGA



Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa AFC Leopards ya Kenya, Dennis Kitambi amesema timu yake iko tayari kukabiliana na Yanga.
Yanga na AFC Leopards zitavaana katika mchezo wa nusu fainali ya mashindano ya SportPesa Super Cup inayoshirikisha klabu za Tanzania na Kenya.
Leopards ilipata nafasi hiyo kwa kuitoa Singida United kwa penalti 5-4, baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.
Kitambi alisema anaamini mchezo huo utakuwa na ushindani kwa timu zote mbili.
"Tunajua Yanga inawakosa wachezaji wake muhimu, lakini sisi tuko tayari kucheza nao katika hali yoyote," alisema Kitambi, aliyewahi kuinoa Ndanda na Azam FC.
Previous
Next Post »