KIMENUKA INDIA : JAJI WA MAHAKAMA KUU AHUKUMIWA - Rhevan Media

KIMENUKA INDIA : JAJI WA MAHAKAMA KUU AHUKUMIWA

India
Image captionJaji CS Karnan
Aliyekuwa hakimu wa zamani wa mahakama kuu nchini India amepelekwa lupango Mashariki mwa mji wa Kolkata, siku moja baada ya kukamatwa kwake Kusini mwa mji wa Tamil Nadu.
Jaji C.S. Karnan alikuwa akijitahidi kujificha kuepuka mkono wa kisheria dhidi yake tangu mahakama kuu ilimhukumu kifungo cha miezi sita jela mnamo mwezi uliopita kwa kosa la dharau dhidi ya mahakama.
Jaji Karnan kwa sasa amevuliwa mamlaka yake ya mahakama. Na inaelezwa kuwa ndiye jaji wa kwanza nchini humo kutoka mahakama kuu kuhukumiwa na kufungwa jela.
Jaji huyo alihojiwa baada ya kumwandikia waraka waziri mkuu,baada ya matamshi yake dhidi ya majaji wenziwe wa mahakama kuu kuwa ni wala rushwa waliopitukia.
Previous
Next Post »