KAIMU MKURUGENZI TAA ASIKILIZA KERO KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA - Rhevan Media

KAIMU MKURUGENZI TAA ASIKILIZA KERO KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


ta1

Wakuu wa Idara wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakijadili masuala mbalimbali walipotembelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Bw. Ramadhan Maleta, katika mwanzo wa Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23 kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
ta2
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhani Maleta akimsikiliza na Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw.Joseph Nyahende (kushoto), wakati wa  kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16 hadi 23. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu, Bw. Mohamed Ally na kushoto ni Mkurugenzi Viwanja vya Mikoa, Bw. Valentine Kadeha.
ta3
Mkuu wa Kitengo cha Usalama katika jengo la kuwasili na kuondokea abiria mashuhuri la VIP kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Leonard Mbogoma (wapili kushoto)akimuelezea jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta alipotembelea jengo hilo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23.
ta4
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Joseph Nyahende akimfafanulia jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta ikiwa ni siku ya kwanza ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23.
ta5
Ofisa Biashara wa JNIA, Bi. Herrieth Nyarusi (kushoto) akizungumza wakati Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta alipotembelea Idara ya Biashara kusikiliza kero na maoni kutoka kwa watumishi, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kulia ni Meneja wa Fedha (JNIA), Bw.Shadrack Chilongani na katikati ni Bw. Godfrey Kanyama.

About bukuku


Previous
Next Post »