HABARI HIVI PUNDE : ASKARI WAWILI WA USALAMA BARABARANI WAUAWA KWA KIPIGWA RISASI KIBTI - Rhevan Media

HABARI HIVI PUNDE : ASKARI WAWILI WA USALAMA BARABARANI WAUAWA KWA KIPIGWA RISASI KIBTI

Picha imefichwa kwa Maadili

Rufiji. Askari Polisi wawili wa kikosi cha usalama wa barabarani wilayani Kibiti ambao majina yao bado hayajatambulika wapigwa risasi na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Msafiri,Kata ya Bungu wakiwa kazini.

Mbali na kupigwa risasi, pia watu hao wamechoma moto gari moja na pikipiki moja za askari hao kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio na kusema anafuatilia.

Tukio hilo limetokea kilomita chache kutoka eneo ambalo waliuawa askari polisi wanane kwa kupigwa risasi katika eneo la Mkengeni walipokuwa wakitoka doria katika Kijiji cha Jaribu.
Previous
Next Post »