ESCROW : SERIKALI YAZUIA MALI ZA SETH SINGH NA RUGEMALIRA - Rhevan Media

ESCROW : SERIKALI YAZUIA MALI ZA SETH SINGH NA RUGEMALIRA

Habari za kuaminika zilizotufikia ni kuwa serikali imezuia mali zote za Singh na Rugemarila . Mali zote zimewekwa chini ya ulinzi mkali na account za benki zimefungwa.

Pia imeelezwa orodha ya waliokwapua pesa za Escrow na kugawana imeongezeka wapo vigogo kutoka wizara ya fedha, taasis za dini, maaskofu, NGOs, na wataanza kuhojiwa kuanzia jumatatu ili nao wafikishwe mahakamani.

Imeelezwa kila aliyehusika atafikishwa mahakama bila kubagua wala kujali nafasi yake katika jamii.

Taarifa zaidi zinaeleza wanaotuhumiwa katika sakata hilo wanakaribia 30.