Kamishna wa Operesheni kutoka mamlaka hiyo, Mihayo Msikhela amesema wamelazimika kuweka kambi wilayani humo kutokana na baadhi ya wananchi kukataa kung’oa miche ya mirungi.
Amesema licha ya kufyeka eka hizo watarudi kuweka kambi katika vijiji vingine vinavyolima mirungi ili kuhakikisha wakulima wanang’oa visiki vya zao hilo kwa hiari yao na kwamba, watakaokaidi agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.
“Viongozi wa wilaya na mkoa wamepiga kelele sana kuhusiana na kilimo hicho na wapo waliong’oa lakini wengine wameendelea kukaidi, tayari wapo waliochukuliwa hatua za kisheria kwa kufungwa miaka 30 jela,” amesema Msikhela.
Amesema hata hivyo katika operesheni hiyo, licha ya kufanikiwa kufyeka hekari nane lakini wameshindwa kumkamata mtu yeyote kutokana na kukuta watoto na wazee katika familia nane walizofyeka mirungi.
Msikhela amesema baadhi ya vijana wameathirika na utumiaji wa dawa za kulevya na hivyo wameshindwa kufanya kazi za kijamii ikiwa ni pamoja na kuhudumia familia.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amesema hadi Julai mwaka jana, vijiji 45 bado vilikuwa vinalima mirungi na kwamba hadi sasa kuna vijiji 13 bado vinalima dawa hizo haramu.
“Wito wangu kuwa wananchi watii sheria na kung’oa wenyewe mibuni ya mirungi ili wasichukuliwe hatua na kwamba tangu mwaka jana hadi sasa tayari watu 4 wamefungwa miaka 30 kwa kujihusisha na kilimo hicho,”amesema Senyamule.
Sign up here with your email