ASKOFU GWAJIMA AGEUZA KIBAO KWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO KWA KULETA SIASA MSIBANI - Rhevan Media

ASKOFU GWAJIMA AGEUZA KIBAO KWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO KWA KULETA SIASA MSIBANI

Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa msibani Moshi amemshukia Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuleta siasa msibani huko Arusha ambapo alimzuia mbunge wa jimbo hilo Godbless Lema kutoongea.

Aidha Gwajima amesema jambo lililofanywa na viongozi wa serikali kukataza Uwanja wa Mashujaa kutumika kuaga mwili wa Marehemu Ndesamburo siyo jambo la busara hata kidogo huku nakimlaumu mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kile alichokisema ni tetesi alizosikia kuwa alitoa maelekezo uwanja huo usitumike na badala yake vitumike Viwanja vya Majengo.
Previous
Next Post »