Gazeti la taifa nchini humo limeandika kuwa mwanaume huyo alilazimika kulipa mahari huku nduguze wakimlazimisha na wakaonya asipofanya hivyo mke wake hatazikwa.
Kosa la kijana huyo kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia wa mwanaume huyo, Irmao do Jovem, ni kutotambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo wakati anaishi naye.
Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na viatu mkewe aliyefariki na kulipa zaidi ya Sh1.7 milioni kama mahari.
''Tulijaribu kuchangisha fedha walizotaka, lakini tuliweza kuchangisha Dola 178 pekee. Hivyo basi ilibidi kuweka ahadi ya kulipa fedha zilizosalia siku ya harusi,''amesema kijana huyo.
Huo ni utamaduni miongoni mwa makabila mengi nchini Msumbiji hususan iwapo mwanaume ataishi na mwanamke bila kufuata sheria na taratibu za ndoa.
Sign up here with your email