ACT - WAZALENDO CHALAANI WALEMAVU KUZUIWA KUONANA NA MKURUGENZI ILALA - Rhevan Media

ACT - WAZALENDO CHALAANI WALEMAVU KUZUIWA KUONANA NA MKURUGENZI ILALA

Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi Chama
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi Chama cha Act Wazalendo, Ado Shaibu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kulaani matumizi ya nguvu ya jeshi la polisi dhidi ya watu wenye ulemavu jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu Kamati ya Programu za jamii, Edina Sunga na kushoto ni Katibu Kamati ya Ulinzi, Nestory Mbena wote wa chama hicho. Picha na Ericky Boniphace 



Chama cha ACT-Wazalendo kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuwazuia kwa nguvu walemavu waliotaka kwenda kumuona Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Ilala.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (Juni 18), Katibu wa Itikadi wa ACT, Ado Shaibu amesema walemavu hao walikusanyika ili kwenda kupeleka malalamiko yao dhidi ya askari wa usalama barabarani kuwakamata na kuwazuia kuingia katikati ya jiji.
"Juni 16, askari polisi waliwavamia, kuwapiga, kuwaswaga na kuwaburuza watu wenye ulemavu," amesema Shaibu.
ACT imemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuomba radhi kwa jumuiya ya watu wenye ulemavu nchini na kuhakikisha vitendo hivyo havirudiwi.

Previous
Next Post »