ZIJUE SIFA NA MAJUKUMU YA MKUU WA MKOA KISHERIA HAPA TANZANIA - Rhevan Media

ZIJUE SIFA NA MAJUKUMU YA MKUU WA MKOA KISHERIA HAPA TANZANIA

Tuanze kwa kutazama majedwali haya na ufafanuzi wake kwa lugha ya kiswahili utafuata..


SEHEMU YA KWANZA: KUHUSU MKUU WA MKOA

- Ni sehemu ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

- Ofisi za Mkuu wa Mkoa zitakuwa kwenye Makao Makuu ya Mkoa husika

- Mkuu wa Mkoa atawajibika chini ya Waziri wa TAMISEMI

2. DHIMA YA KAZI HII

Kuhakikisha kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanapatikana kutokana na huduma bora za ushauri na uratibu ambazo zinajenga mazingira bora kwa Serikali za Mitaa na wadau kutoa huduma inayotarajiwa.

3. MAJUKUMU NA KAZI ZA MKUU WA MKOA

- Kuhakikisha uwepo wa Haki na Sheria kk mkoa

- Kuongoza na kusimamia operesheni za Maafa na Kufariji

- Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC), Mkuu wa Mkoa atawajibika kufanya jitihada za kuhakikisha kutimizwa kwa sera za serikali juu ya Mkoa husika.

- Kufanya yale yote yatakayosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mkoa kwa ushirikiano na serikali za mitaa.

4. ELIMU

Mkuu wa Mkoa itampasa awe na Elimu Ngazi ya Shahada(Degree) au inayoshabihiana na hiyo kutoka kwenye Taasisi ya Elimu inayotambulika.

5. UELEWA

Mkuu wa Mkoa atapaswa awe ni mwenye ufahamu kuhusu Utawala wa Sheria, Utawala bora, Kanuni za Haki Asilia (Natural Justice), Sera na taratibu zake, Uongozi na Utawala pamoja na masuala yote ya msingi ktk utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.

6. UJUZI

Kimsingi Mkuu wa Mkoa anapaswa kuwa na stadi zote za uongozi;

Ujuzi wa kujenga umoja, ujuzi wa kutatua changamoto, ujuzi wa kutoa ushauri nasaha, ujuzi wa maridhiano, ujuzi wa kuhimili msongo/mihemuko, sambamba na ujuzi kuhusu mahusiano ya umma na uwezo wa kuzungumza vizuri mbele za watu.

7. SIFA BINAFSI

Aonyeshe uwezo wa kutunza siri, kufanya maamuzi yenye tija, kufanya kazi pasipo mashinikizo, uelewa kuhusu mwenendo wa siasa na tamaduni za jamii, awe na heshima, mbunifu, mtenda haki, bila kusahau kuheshimu miiko ya kazi.

8. UZOEFU

Ni lazima Mkuu wa Mkoa awe ni mtu mwenye uzoefu kuhusu masuala ya utawala/siasa usiopungua Miaka 10.

9. MSHAHARA

Mkuu wa Mkoa atalipwa kiwango cha mshahara kwa taratibu zilizoainishwa na Ofisi ya Utumishi (kwa sasa salary scale yake ni LSS(P) 4).

Asanteni.
Previous
Next Post »