Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema wamekubaliana na Rais Jacob Zuma kupeleka walimu kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufundisha Kiswahili.
Rais Magufuli amesema hayo leo (Alhamisi) wakati wa hafla kutia saini mikataba ya ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo.
Amesema yeye na Rais Zuma wameshakubaliana kuhusu hilo na kwamba walimu hao watakwenda nchini humo baada ya taratibu muhimu kukamilika.
Rais Zuma amewasili nchini tangu jana usiku kwa ziara ya siku tatu kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais Magufuli.
Sign up here with your email