WAGONJWA WAACHA VITANDA NA KUOMBA KUPIGA PICHA NA MHE . MBOWE - Rhevan Media

WAGONJWA WAACHA VITANDA NA KUOMBA KUPIGA PICHA NA MHE . MBOWE


Wagonjwa waacha vitanda na kuomba kupiga picha na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa Hai Mhe.Freeman Mbowe

Mhe.Mbowe jana alitembelea Hospitali ya Wilaya ya Hai pamoja na kuwasalimia wagonjwa waliopo hospitalini hapo ndipo gumzo lilipotkea baada ya sauti za wagonjwa kusikika zikisema "KAKA ,KAKA" kumbe walikua wakimuita Mhe.Mbowe wakihitaji angalau kumshika mkono nakupiga picha pamoja nae.

Mhe.Mbowe aliongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai Mhe.Helga Mchomvu pamoja na Katibu wake Irene Lema
Mhe.Mbowe alitembelea Maabara ya hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo Mhe.Mbowe alitembelea shule za sekondari katika kata ya Machame Kaskazini,Masama kusini na kata ya Boma yang'ombe

Takribani siku kadhaa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe.Freeman Mbowe alikiwepo Jimboni kwake na alikua na ziara mbali mbali.
Previous
Next Post »