WAFAHAMU WASANII WANAOINGIZA PESA NYINGI AFRIKA KWA MUJIBU WA FORBES - Rhevan Media

WAFAHAMU WASANII WANAOINGIZA PESA NYINGI AFRIKA KWA MUJIBU WA FORBES

Jarida la Forbes Africa la mwezi May 2017 limeandaa list ya wasanii 10 wanaoingiza pesa nyingi zaidi Africa.



List hiyo ambayo inaongozwa na msanii wa Nigeria, Akon na nafasi ya pili ikichukuliwa na producer na msanii wa Afrika Kusini, Black Coffee imendaliwa kwa vigezo vya thamani ya endorsement wanazozipata, umaarufu, viwango vya show zao wanazofanya, mauzo, tuzo, watazamaji wao kwenye chaneli za YouTube, kutokea kwenye magazeti, kuwa na ushawishi mkubwa kuliko wengine, uwekezaji na uwepo wao katika mitandao ya kijamii.

1.AKON

Akon anaingia kwenye list hii kutokana na mauzo ya albumu zake akribani milioni 35 zilizouzwa kila pande ya dunia, kingine kikubwa ni kwamba Akon ameshajinyakulia grammy tano huku akiwa ameingiza ngoma 45 katika chati za ya Billboard hot 100.

2. BLACK COFFEE, AFRIKA KUSINI

Maarufu sana kutokana na tuzo ambazo amewahi kujishindia kama BET, wengi wanamfahamu kwa jina kamili la Nkosinathi Maphumulo , kubwa zaidi Black Coffee, ameingia kwenye albumu mpya ya Drake ‘More Life’ ambayo inafanya vizuri sokoni.



3. HUGH MASEKELA

Alizaliwa Witbank, Mashariki mwa Johannesburg, Hugh Masekela ashafanya takriban albumu 43 ambazo zote hizo aliwahi kuperforme na wasanii wakubwa kama Marvin Gaye, Stive Wonder, Miriam Makeba na wengine kibao.

4. DON JAZZY, NIGERIA

Ni msanii pia ni producer kutoka nchini Nigeria ambaye amejibebea umaarufu kutokana na mafanikio makubwa katika game ya muziki Afrika mpaka Marekani ambapo alifanikiwa kuja na label yake ya  Mavins ambayo nayo imebeba vichwa vingi vikubwa vinavyofanya vizuri Afrika, Do Jazzy alianza tasnia ya muziki tangu yuko mdogo kanisani mpaka kufikia hatua hii aliyokuwa nayo sasa. Pia msanii kutoka kwenye label yake ya Mavins, Tiwa Savage alisaini katika label ya Jay Z, Roc Nation.



5. TINASHE, ZIMBABWEAN-AMERICAN

Maarufu na ngoma kama ya “2 On aliyomshirikisha School Boy” pamoja na “How long” ya Davido, Tinashe ni mchanganyiko Mzimbwabwe pamoja na America, vilevile ni mwandishi mzuri wa nyimbo, muimbaji, muigizaji pamoja na dancer. Alishashinda tuzo kibao kupitia wimbo wake wa “2 On”. Tinashe aliingia kwenye listi ya kuwa mwanamke wa kwanza kutokea katika jarida la Play Boy bila kukaa utupu.

6. JIDENNA, NIGERIAN-AMERICAN

Mzee wa Classic, anajulikana kama Jidenna Theodore Mobisson, mbali na kuwa maarufu katika tasnia ya muziki, Jiddena angekuwa ni moja ya masound Engineer, amejizolea umaarufu na ngoma yake ya Classic Man, Yoga, Long Live Chief na zingine kibao.



7. WIZKID, NIGERIA

Moja ya wasanii wa Afrika wanaofanya vizuri duniani na kugusa kila mioyo ya wapenda muziki, ameingia kwenye tuzo nyingi kubwa duniani kupitia wimbo wa “One Dance” alioshirikishwa na Drake pamoja na “Come Closer” anayotamba nayo kwa sasa.

8. DAVIDO, NIGERIA

Ni mmoja kati ya wasanii ambao wamepigana sana kufikia hatua ambayo yupo nayo sasa akiwa na ngoma nyingi kali na kutengeneza njia kibao kwa muziki wa Afrika kuchomoza zaidi. Alishapiga kolabo na msanii kutoka Bongo, Diamond platnumz.

9. SARKODIE, GHANA

Alianza kama underground rapper katika tasnia ya muziki wa kiafrika mpaka kufikia hatua ya mghana wa kwanza kushinda tuzo ya BET, maarufu na ngoma “No kissing Baby”, “Pain Killer”.

10. OLIVER MTUKUDZI, ZIMBABWE

Albumu 65 zikiwa kwenye tasnia yake ya muziki, katika miaka yake 41 ya muziki, nyimbo zake zimekuwa zikichezwa duniani kote, maarufu zaidi masikioni mwa mashabiki na kibao cha “Neria”
Previous
Next Post »