SAFARI YA MAJERUHI WATATU WA LUCKY VICENT KWENDA MAREKANI YAANZA - Rhevan Media

SAFARI YA MAJERUHI WATATU WA LUCKY VICENT KWENDA MAREKANI YAANZA




Arusha. Safari ya kwenda Marekani kwa matibabu wanafunzi watatu wa Shule ya Lucky Vicent imeanza muda huu baada ya kupandishwa kwenye ndege maalum ya shirika la Samaritan la Marekani na watatumia saa 20 kufika nchini humo.
Majeruhi hao ambao walikuwa wamelazwa hospitali ya Mount Meru ni Jofrey Tarimo, Doreen Mshana na Saida Awadh wameagwa leo jijini Arusha kwa ajili ya kwenda kwenye matibabu hayo wakiwa na  wazazi wao na muuguzi mmoja.

Previous
Next Post »