Dar es Salaam. Nyota wa Serengeti Boys watoa ahadi kwa Watanzania ya kufanya vizuri katika mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana walio na umri chini ya miaka 17 itakayochezwa Gabon kuanzia Mei 15-28.
Serengeti Boys ipo kambini Cameroon ikijiandaa na mashindano hayo kwa lengo la kuingia nusu fainali ili ipate tiketi ya kucheza Kombe la Dunia nchini India, Oktoba 6 hadi 28.
Mshambuliaji Yohana Mkomola amesema wanahamu mkubwa wa kucheza Kombe la Dunia na ndoto hiyo itafikia kama watafanya vema Gabon.
“Maandalizi yametupa nguvu kila mchezaji kwa kuamini kuwa tutafanya vizuri, tumekuwa na umoja wenye lengo moja la kufanya vizuri,” alisema Mkomola.
Naye Kelvin Kayego alisema ni wakati wa Tanzania kufanya vizuri kwenye mashindano hayo maana kila miaka imekuwa mataifa mengine hivyo watajitahidi kufanya vizuri kwa manufaa ya Taifa.
“Watanzania watuombee na kuendelea kutusapoti mpaka kufika kwetu hapa haikuwa kazi nyepesi, umoja tulio nao na kiwango tulicho kionyesha kwenye mechi zilizopita kitaendelea kwenye mashindano” alisema Kayengo.
Sign up here with your email