NUSURU AENDE JELA KWA KUFANANA NA MESSI - Rhevan Media

NUSURU AENDE JELA KWA KUFANANA NA MESSI




London, England.Kufanana na Lionel Messi nusura kumpeleke jela mwanafunzi wa Kiirani baada ya kuzua vurugu kwa  mashabiki waliotaka kupiga naye picha mitaani.
Mwanafunzi huyo, Reza Parastesh anayefanana na Messi aliwavutia mashabiki wengi wakiomba kupiga naye picha 'selfies' jambo lililosababisha vurugu na kulazimisha polisi kumkata na kumpeleka kituo cha polisi.
Pia, gari la Paratesh (25) liliongozwa na trafiki kutoka katika kituo hicho kutokana na mashabiki wengi wa Iran kuvutiwa naye.
Paratesh alisema: “Sasa watu wananiona mimi kama Messi wa Iran na wananitaka mimi nifanye kila kitu anachofanya. Ninapojitokea sehemu yoyote watu wote wanachanganyikiwa.
“Nina furaha sana kuona jinsi ninavyoweza kuwapa furaha watu wengi.”
Parastesh kwa sasa anabadilisha nywele zake na kufanana na Messi na mara kadhaa anapopita mitaani anavaa jezi ya Barcelona.
Previous
Next Post »