NHC YAPATA MWAROBAINI WA NYUMBA ZINAZOCHELEWA KUUZWA - Rhevan Media

NHC YAPATA MWAROBAINI WA NYUMBA ZINAZOCHELEWA KUUZWA




Mwenyekiti wa NHC, Blandina Nyoni
Mwenyekiti wa NHC, Blandina Nyoni 

Dodoma. Shirika la Nyumba Nchini (NHC) linaanza utaratibu wa kujenga nyumba kulingana na mahitaji ya eneo husika ili kukabiliana na tatizo la nyumba zilomaliziwa kujengwa kuchelewa kuuzwa.
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi ya nyumba za shirika hilo Wilaya ya Kongwa na Iyumbu mjini Dodoma, Mwenyekiti wa NHC, Blandina Nyoni amesema kuwa hali hiyo inatokana na baadhi ya nyumba kushindwa kupata wateja.
“Hivi sasa tutakuwa tukiangalia mahitaji ya eneo husika kabla ya kuanza mradi wa ujenzi,”amesema Nyoni.
 Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ujenzi wa shirika hilo, Haikamen Mlekio amesema  kuwa  mradi wa ujenzi wa nyumba 44 Wilaya ya Kongwa ulikamilika Desemba 14 mwaka jana.
Hata hivyo amesema kuwa nyumba 13 tu ndizo zimepata wateja ambazo kati ya hizo 10 zimenunuliwa na Halmashauri ya Kongwa.








Previous
Next Post »