MSANII JAGUAR AMRUDIA MUNGU BAADA YA KUKARIBIA KUUKOSA UBUNGE - Rhevan Media

MSANII JAGUAR AMRUDIA MUNGU BAADA YA KUKARIBIA KUUKOSA UBUNGE


Mwana muziki kutokea nchini Kenya, maarufu kama Jaguar, ameamua kumrudia Mungu wake mara baada ya kuyapitia magumu katika siasa.
Kwenye kura za maoni za kumwezesha kugombea ubunge nchini Kenya, Jaguar alitajwa kupita kwa wingi wa kura dhidi ya mpinzani wake Maina Kamanda, lakini baadaye taarifa zikatolewa kuwa kuna makosa yalifanyika, hivyo mpinzani wake Maina Kamnada ndiye amepita katika kura hizo za maoni.
Kufuatia tukio hilo, Jaguar alionekana amekosa raha na kuangusha machozi mbele za watu waliokuwepo, na ndipo watu hao walimshauri amuunge mkono mshindi ambaye ni Maina iliwaweze kufanya naye kazi kwa pamoja.
Jaguar alisema kwamba “Ninaamini Mungu ndio kila kitu kwangu, hata kama kuna mchezo unachezeka, ninaamini malipo yake ni hapa hapa duniani. Kikubwa ninachokifanya ni kumshitakia Mungu wangu,” Kwa sasa msanii huyo ameonekana akifanya maombi pia akikutana na wachungaji akiwemo Margaret Kenyatta.
Hata hivyo, baada ya maandamano makubwa ya wafuasi wa Jaguar, mwenyekiti wa chama cha Jubilee, amemkabdihi cheti cha ushindi wa kura za maoni msanii huyo, hatua mabayo itamuwezesha kugombea ubunge katika uchaguzi ujao nchini Kenya.
Previous
Next Post »