Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limetangaza jumla ya mabondia ishirini (20) kati yao wanaume kumi na watano (15) wanawake watano (5) kuunda kikosi cha timu ya taifa ya ngumi 2017.
Uteuzi huo umefanywa na kamati ya ufundi ya BFT ikiwa chini ya Kocha David Yombayomba kocha Mkuu wa timu ya ngome akishirikiana na makocha wa timu zote zilizoshiriki mashindano ya ngumi ya taifa yayomalizika 30/04/2017 Kawe, Dar es salam.
Uteuzi huo umezingatia uwezo wa sasa wa kucheza mchezo wa ngumi, umri unaokubalika kwa mujibu wa sheria za chama cha ngumi cha dunia (AIBA) na tabia binafsi ndani na nje ya ulingo.
Majina ya mabondia na uzito wao ni kama ifuatavyo:-
- Light Fly weight 49 Kgs. Herman Richard (Ngome)
- Fly weight 52 Kgs. Ibrahim Aballah (Urafiki) George Costantino (Ngome)
- Bantam weight 56 Kgs. Ezra Paulo ( Ngome)
- Light weight 60 Kgs. Ismail Galiatano (Ngome) king Lucas (Kigoma)
- Light welter 64 Kgs Mohamed Juma (Ngome) kassim Seleman (Ngome)
- Welter 69 Kgs. Said Ramadhan (JKT) Haruna Hussein (JKT)
- Middle weight 75 Kgs Seleman Kidunda
- Light heavy weight 81 Kgs Yusuph Changarawe
- Heavy Weight 91 kgs. Haruna swanga (Ngome)
- Super Heavy weight 91+ Mhina Morris (Ngome) Alex Sitta (JKT)
Aidha wanawake waliochaguliwa ni Sara Andrew ( Ngome), Grace Joseph (JKT), Siwatu Eliuta (JKT), Sarafina James (JKT) na Aliskunda Jonas (Kigoma)
Jumatatu ya Tarehe 8/5/2017 shirikisho litaanza hatua ya kuwaombea ruhusa kutoka kwa waajili wao ili kuanza mazoezi haraka iwezekanavyo ajili ya kushiriki mashindano ya Ubingwa wa Afrika yatakayofanyika Congo Brazzaville 25/05-04/06/2017.
Pia baadhi yao watakwenda kushiriki mashindano ya Afrika mashariki yatakayofanyika Kampala Uganda mwishoni mwa mwezi huu.
Shirikisho la ngumi BFT linawapongeza kwa jitihada walizofanya hadi kufikia hatua kubwa ya kuchaguliwa kuwa wachezaji wa timu ya taifa ya ngumi na linawaomba kuongeza bidii katika mazoezi na kuwa wavumilivu na moyo wa kizalendo ili kufikia mafanikio ya uwakilishi wenye tija katika mashindano ya kimataifa watakayokwenda kutuwakilisha Taifa.
Makore mashaga
Katibu Mkuu(BFT)
Sign up here with your email