Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya wiki moja.
Mkanda mfupi wa video, unamuonyesha Bw Buhari akizungumza na watu, baada ya kutoka msikitini kwa swala ya Ijumaa katika Ikulu ya Rais.
Maafisa wake wa mawasiliano pia wamepakia picha zake akitembea kutoka msikiti huo katika ikulu ya rais kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Kumekuwepo na wasiwasi kuhusiana na afya ya Rais huyo, kwani hajaonekana hadharani tangu aliporejea Nigeria kutoka kwa ziara ya matibabu ya wiki saba nchini Uingereza, alipokwenda kutibiwa ugonjwa ambao bado haujajulikana.
Pia hajahudhuria mikutano mitatu ya baraza la mawaziri, na hakuhudhuria maombi ya ijumaa msikitini juma lililopita.
Lakini washauri wake wanasema kwamba, alikuwa akipumzika huku akifanya kazi akiwa nyumbani.
Sign up here with your email