KIMENUKA : TFDA YAFUNGIA MACHINJIO 26 DAR - Rhevan Media

KIMENUKA : TFDA YAFUNGIA MACHINJIO 26 DAR


 Tokeo la picha la MACHINJIO YA NG'OMBE






Dar es Salaa. Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imeyafungia machinjio 26  kati ya 55 jijini hapa katika Manispaa za Ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amesema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari kuwa ukaguzi ulianza Mei 2-12 na kuwahusisha wadau wote muhimu wakiwemo Bodi ya Nyama na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
"Lengo la ukaguzi huo ulikuwa kuangalia utekelezaji wa Sheria ya Chakula, Dawa ya Vipodozi... Ulifanyika usiku kwa machinjio ya ng'ombe na asubuhi na mchana kwa machinjio ya kuku na nguruwe," amesema Sillo.
Amesema katika machinjio 26,  moja ni ya ng'ombe, 14 nguruwe na 11 ya kuku.

Previous
Next Post »