JELA MAISHA KWA UBAKAJI - Rhevan Media

JELA MAISHA KWA UBAKAJI



Hai. Mahakama ya Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro imemuhukumu kifungo cha maisha, kuchapwa viboko vitano na kulipa fidia ya Sh500,000  Nemence Dominik(25) mkazi wa kijiji cha Usari Narumu baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka sita ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza.
Hukumu hiyo ilitolewa leo (Jumanne) na Hakimu mkazi mfawidhi  wa Mahakama hiyo, Arnold Kirekiano baada ya kuridhika na ushahidi wa watu watatu uliotolewa Mahakamani hapo usioacha shaka, ukiwamo kutoka kwa  mhanga mwenyewe,daktari wa Wilaya, na mzazi wa mtoto huyo.
Inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume kinyume na kifungu Na.131 (A)(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 12 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Mwendesha mashtaka wa polisi, Elisha Mollel alidai  kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 14, 2016  saa 12 jioni katika kijiji hicho kwa kumbaka mwanafunzi wa miaka (6) na kumsababishia maumivu makali mtoto huyo. 









Previous
Next Post »