Dar es Salaam.Mahakama ya Hakimu Kisutu Julai 31,2017 itatoa hukumu katika kesi inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake watatu.
Katika kesi hiyo Gwajima anakabiliwa na shtaka la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi.
Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha baada ya mashahidi wa upande wa mashtaka na utetezi kutoa ushahidi wao na kuufunga.
Upande wa mashtaka unawakilishwa na mawakili, Shedrack Kimaro na Joseph Maugo hukumu upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala.
Sign up here with your email