FAIDA YA KUVAA SOCKS MIGUUNI WAKATI WA TENDO LA NDOA - Rhevan Media

FAIDA YA KUVAA SOCKS MIGUUNI WAKATI WA TENDO LA NDOA


Utafiti uliofanywa na jopo la watafiti wenye utaalam wa masuala ya uhusiano na saikolojia wa Chuo kikuu cha Wageningen nchini Uholanzi umebaini faida za kushiriki tendo la ndoa ukiwa umevaa socks miguuni.

Bila shaka utakuwa umewahi kuona picha za watu wanaotengeneza taswira ya wanandoa wakiwa kitandani na socks miguuni. Huenda waliuamini utafiti huu na baada ya kujaribu wakaona unazaa matunda wayatakayo.

Katika utafiti huo, waligundua kuwa uvaaji wa socks miguuni kwa wanaume na wanawake kunaongeza ari zaidi na uwezekano wa kufika kileleni kwa haraka na mshindo wa nguvu zaidi kutoka 50% (kabla ya kuvaa socks) na 80% (baada ya kuvaa socksi).

Utafiti huo ulizaliwa kutoka kwenye ule wa awali ulifanywa mwaka 2011 na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Watafiti wa Johns Hopikins walikuwa wakijaribu kuusoma ubongo wa binadamu wakati akishiriki tendo la ndoa, kujua madhara ya kisaikolojia na kimwili anayoyapata wakati anapofika kileleni.

Wakati wakiendelea na na zoezi hilo, watu waliokuwa wanatumika kama sampuli wakifanya mapenzi, walilalamikia hali ya ubaridi ndani ya chumba chenye ‘scanner’ ya ubongo. Ndipo watafiti hao walipoamua kuwavalisha socks miguuni. Ghafla uwezo wao katika tendo hilo ulipanda kutoka 50% hadi 80% za kukifikia kilele kwa kishindo zaidi.

Nao watafiti wa Chuo Kikuu cha Wageningen wamebaini kuwa kuiweka miguu pekee kwenye hali ya joto kupitia socks, kunaongeza kwa asilimia za za ziada 30.
Previous
Next Post »