Dar es Salaam. Ecobank imewaondoa hofu wateja wake na kusema kuwa haina dhamira ya kusitisha shughuli zake hapa nchini .
Hata hivyo benki hiyo imekiri kwamba kumekuwa na ongezeko la wateja kushindwa kurejesha mikopo yao ya mwaka jana.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank, Raphael Benedict amesema benki hiyo inachukua hatua muhimu ili kuwezesha urejeshaji wa mikopo hiyo ndani ya miezi mitatu.
Kuhusu kutositisha shughuli zake nchini, Benedict amesema hiyo ilikuwa ahadi ya Ecobank tangu walipoanza kufanya shughuli zake hapa nchini miaka saba iliyopita na kwamba wataendelea kutumiza ahadi hiyo.
Sign up here with your email