ZIMA MOTO WALIA UFINYU WA RASILIMALI - Rhevan Media

ZIMA MOTO WALIA UFINYU WA RASILIMALI

Tokeo la picha la JESHI LA ZIMAMOTOKamishina Jenerali wa jeshi hla Zimamoto, Thobias Andengenye akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Ephrahim Bahemu 

Dar es Salaam. Jeshi la Zimamoto nchini linakabiliwa na ufinyu wa rasilimali watu na vitendea kazi katika huduma jambo ambalo linasababisha kuwa na vituo katika wilaya tisa tu kwa nchi nzima.
Hayo yamebainishwa leo  na Kamishina Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye ambaye amesema uchache wa watu na vifaa katika jeshi hilo usababisha baadhi ya wananchi kutofikiwa wanapokuwa wameripoti taarifa za moto hususani mikoani.
"Jeshi leo lina magari ya zimamoto yasiyozidi 100 na mahitaji kwa nchi hii ni walau magari 300 ndipo kila wilaya itaweza kuwa gari hilo. Serikali bado inafanya juhudi za kuhakikisha magari hayo yanapatikana lakini pia inapaswa kuajili watumishi wapya ili kuweza kuzifikia wilaya zote," amesema Andengenye.







Previous
Next Post »