Mtaalamu wa mada za kemikali wa Marekani amesema serikali ya Washington ilitumia ripoti bandia kutekeleza mashambulizi ya makombora ya tomahawk dhidi ya Syria.
Profesa Theodore Postol, Mtaalamu wa Sera za Usalama wa Taifa na Teknolojia nchini Marekani amewasilisha ripoti yenye kurasa 6, inayothibitisha kuwa Washington ilitumia taarifa iliyokuwa na dosari, kama kigezo cha kuituhumu serikali ya Damascus kwamba imetekeleza shambulizi la silaha za kemikali dhidi ya eneo la Khan Sheikhoun.
Amesema: "Ripoti iliyotumiwa na Ikulu ya White House kuwa gesi ya sumu ya sarin ilipatikana katika eneo la tukio na hivyo kuihusisha moja kwa moja serikali ya Damascus kuwa imehusika na shambulizi hilo la silaha za kemikali imejaa dosari, na hivyo tuna wasi wasi iwapo White House imekuwa ikitumia ripoti za namna hii huko nyuma au la."
Marekani ilivurumisha makombora 59 kutokea meli zake mbili za kivita katika bahari ya Mediterania na kukishambulia kituo cha jeshi la anga la Syria katika eneo la Shayrat katika mkoa wa Homs na kuua watu tisa wakiwemo watoto wanne na kujeruhi wengine kadhaa.
Rais Donald Trump wa Marekani aliagiza kutekelezwa mashambulizi hayo, kwa kisingizio bandia kuwa serikali ya Syria iliua watu zaidi ya 80 kwa hujuma ya silaha za kemikali dhidi ya raia wa nchi hiyo, suala ambalo limekanushwa vikali na Damascus.
Sign up here with your email