WANAJESHI KENYA WAWAUA WAPIGANAJI 50 WA AL-SHABAB - Rhevan Media

WANAJESHI KENYA WAWAUA WAPIGANAJI 50 WA AL-SHABAB

Wanajeshi wa Kenya wamewaua takriban wapiganaji 50 wa kundi la al-Shabab nchini Somalia
Image captionWanajeshi wa Kenya wamewaua takriban wapiganaji 50 wa kundi la al-Shabab nchini Somalia
Jeshi la Kenya linasema kuwa limewaua zaidi ya wapiganaji 50 wa Al-Shaabab katika oparesheni iliyofanywa Kusini mwa Somalia.
Jeshi hilo lilisema lilinasa shehena ya silaha na risasi na kuharibu kabisa kambi ya wapiganaji hao katika eneo la Badhaadhe katika Lower Juba.
Hadi sasa Al Shaabab hawajasema lolote.
Maelfu ya wanajeshi wa Kenya wanahudumia nchini Somalia chini ya mwavuli wa Muungano wa Afrika.
Wanajeshi wa Kenya wakipiga doria
Image captionWanajeshi wa Kenya wakipiga doria
Al Shaabab hufanya mashambulizi ya mara kwa mara kwenye mpaka na Kenya na pia kwenye kambi za wanajeshi wa Kenya walioko Somalia.
Previous
Next Post »