NEW DELHI, India. Mtanzania (65) ambaye jina lake halijafahamika, ameporwa mkoba wenye dola za Kimarekani 6,000 (sawa na Sh13.4 milioni)akiwa nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu ya mjukuu wake.
Fedha alizoporwa ni kwa ajili ya matibabu ya mjukuu wake aliyelazwa jijini New Delhi, India, gazeti la mtandaoni la The Times of Indialimeripoti leo.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mwanamke huyo akiwa na familia yake aliporwa mkoba wake na watu wawili wakati akielekea hoteli iliyopo maeneo ya Karol Bagh, katikati ya jiji la New Delhi, Ijumaa, wiki iliyopita.
Sign up here with your email
