MAREKANI KUIMARISHA VIKWAZO DHIDI YA KOREA KASKAZINI - Rhevan Media

MAREKANI KUIMARISHA VIKWAZO DHIDI YA KOREA KASKAZINI

Taifa la Korea kaskazini limekuwa likitoa picha kuhusu zoezi la kijeshi

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionTaifa la Korea kaskazini limekuwa likitoa picha kuhusu zoezi la kijeshi
Mamlaka ya rais Donald Trump imewaelezea maseneta wote 100 wa bunge la taifa hilo kuhusu tishio la Korea Kaskazini na kubaini mikakati ya kuishinikiza Pyongyang kupitia vikwazo vya kiuchumi na vile vya kidiplomasia.
Lengo ni kuilazimu Korea Kaskazini kusitisha mpango wa makombora ya masafa marefu pampja na ule wa Kinyuklia.
Mwandishi wa BBC mjini Washington anasema kuwa mkakati muhimu pia utakuwa kuirai China kuishinikiza Pyongyang.
Maseneta wa Marekani walielezwa na mamlaka ya rais Trump kuhusu tishio linaloletwa na Korea KaskaziniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMaseneta wa Marekani walielezwa na mamlaka ya rais Trump kuhusu tishio linaloletwa na Korea Kaskazini
Seneta mmoja alisema kuwa habari hiyo kuhusu Korea Kaskazini ilikuwa muhimu sana.
Taarifa iliotolewa kwa niaba ya wizara ya Ulinzi na ile ya kigeni ilisema kuwa Marekani bado itaendelea na mazungumzo lakini imejiandaa kujitetea pamoja na washirika wake.
Awali kamanda mkuu wa Marekani katika eneo la Pacific alitetea kupelekwa kwa mfumo wa silaha za kisasa nchini Korea Kusini.
Hali ya wasiwasi imepanda huku kukiwa na hofu kwamba Korea Kaskazini inapanga kujaribu makombora mapya.
''Marekani inataka uthabiti na kutoenea kwa silaha za kinyuklia katika rasi ya Korea'', ilisema taarifa ya pamoja iliotolewa na waziri wa maswala ya kigeni REx Tillerson, waziri wa Ulinzi Jim Mattis na Mkurugenzi wa maswala ya ya ujasusi Dan Coats.
Previous
Next Post »