MAKOMANDOO WAACHA GUMZO - Rhevan Media

MAKOMANDOO WAACHA GUMZO

Askari wa kikosi cha makomandoo cha Jeshi la
Askari wa kikosi cha makomandoo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakionyesha umahiri wao katika sherehe za miaka 53 ya Muungano zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Dodoma. Ikiwa ni mara ya kwanza kwa sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuadhimishwa mjini Dodoma, huku zikipambwa na shamrashamra mbalimbali ikiwamo gwaride lililoandaliwa na majeshi, Kikosi cha Makomandoo ndicho kilichosababisha gumzo kwa mamia ya wahudhuriaji.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na mamia ya Watanzania wakiwamo viongozi waliopo madarakani na  wastaafu, jana walijitokeza kushuhudia sherehe za miaka 53 ya muungano huo zilizofanyika katika Uwanja vya Jamhuri mjini hapa.
Kila aliyeingia uwanjani hapo baada ya milango kufunguliwa kuanzia saa 12:30 asubuhi, alipewa bendera ndogo ya Taifa kwa ajili kusherehesha shughuli hiyo.
Kuanzia saa 1:00 asubuhi viongozi mbalimbali walianza kuingia uwanjani hapo kabla ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuwasili akifuatiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na baadaye Rais John Magufuli aliyefika saa 3:15 asubuhi.
Sherehe hizo zilipambwa na maonyesho mbalimbali ya kijeshi yakiwamo ya kikosi cha makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikosi cha mbwa cha Jeshi la Polisi, halaiki, na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Licha ya matukio hayo yote kuwa na msisimko mkubwa, makomandoo wa JWTZ walitia fora na tukio lililowaacha wengi vinywa wazi ni lile la baadhi yao kuwabeba wengine kwa kutumia meno. Pia, wananchi waliweka mikono vinywani pale waliposhuhudia makomandoo wawili wakivuta kwa kamba lori kubwa la jeshi aina ya Iveco lenye uzito wa tani saba.









Previous
Next Post »