MAKAMBA : CHANGAMOTO 12 ZA MUUNGANO ZIMETATULIWA - Rhevan Media

MAKAMBA : CHANGAMOTO 12 ZA MUUNGANO ZIMETATULIWA

Waziri wa nchi anayeshughulikia masuala ya
Waziri wa nchi anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira January Makamba. 
Dodoma. Waziri wa nchi anayeshughulia masuala ya Muungano na Mazingira January Makamba amesema kuwa changamoto za Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka 15 mwaka 2006 hadi kufikia changamoto  tatu mwaka huu.
Tanzania itaadhimisha miaka 53 ya Muungano, wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, wiki ijayo.
Waziri Makamba amezungumza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari.
Mhe. Makamba amezitaja changamoto zilizobakia kuwa ni pamoja na usajili wa vyombo vya moto unaorahisisha kusafirisha magari kutoka Zanzibar kwenda Bara na  kutoka Bara kwenda Zanzibar na kusema kuwa swala hili linafanyiwa kazi kwa kumalizwa  kwa taratibu za kisheria.

Previous
Next Post »