BBC KUFUFUKIA KWA BAYERN - Rhevan Media

BBC KUFUFUKIA KWA BAYERN


Madrid, Hispania .Real Madrid  watakuwa wageni wa Bayern Munich kwenye Uwanja wa Allianz leo katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Ujerumani Real 'Los Blancos' ilishinda mabao 4-0  na kusonga mbele kwa fainali.
Katika siku za karibuni Gareth Bale, Karim Benzema na Cristiano Ronaldo wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na watatu hao kupoteza uwezo wao wa kufunga na kuisaidia timu.
Kocha Zinedine Zidane ameshindwa kupata matokeo mazuri kutoka wa washambuliaji wake watatu msimu huu.
Uwezo wa Bale katika kufunga umekuwa chini zaidi kutokana na kukosa nafasi kadhaa za wazi katika mechi ya watani wa jadi dhidi ya Atletico Jumamosi iliyopita.
Hata hivyo, Zidane atalazimika kuwaanzisha BBC leo mjini Munich.
Lewandowski, Muller wapo fiti
 Washambuliaji Bayern Munich, Robert Lewandowski na Thomas Muller amereja kikosini tayari kuivaa Real Madrid.
Washambuliaji hao walishindwa kufanya mazoezi na wenzao juzi kutokana na sumbuliwa na majeraha waliyopata wakati wa mechi dhidi ya Dortmund iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Muller pia, aliungana na wenzake katika kujiandaa na mechi hiyo dhidi Real Madrid.
“Tumejianda vyema. Nilishiriki kwenye mazoezi ya kawaida na wenzangu na hii ni ishara njema,” alisema Muller.
Kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti alisema Lewandowski amefanya mazoezi mepesi na huenda akacheza kwenye mechi hiyo.
Previous
Next Post »