27 WANUSURIKA KIFO BAADA YA BOTI KUZAMA RUFIJI - Rhevan Media

27 WANUSURIKA KIFO BAADA YA BOTI KUZAMA RUFIJI



Rufiji. Mtu mmoja anahofiwa kufa wakati watu wengine 27 wakinusurika  baada ya boti waliyokuwa wakisafiria  kuzama katika mkondo wa maji wa bahari ya Hindi wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
Anayehofiwa kufa ni mkazi wa kijiji cha Mbwera aliyetambulika kwa jina la Rukia Chobo (35)
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Onesmo Lyanga alithibitisha kutokea tukio hilo na kusema jitihada za kumsaka mwanamke huyo zinaendelea.

Previous
Next Post »