Katika juhudi za kuongeza idadi ya watu inayoendelea kupungua, nchini Uhispania sasa serikali imeamua kumteua waziri wa masuala ya ngono.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Mariano Rajoy amethibitisha uteuzi wa Edelmira Barreira kuwa afisa mkuu wa masuala ya ngono.
Hatua ya kubuni wizara nzima ya maswala ya ngono na mahaba huko Uhispania imetokana na hofu waliyo nayo wanasiasa.
Wakati kwengineko duniani watu wana hofu kwamba idadi ya watu nchini mwao inaongezeka kushinda rasilmali zilizopo , huko Spain hofu ni kwamba idadi ya watu inapungua, tena kwa kasi ya kutisha.
Mbali na kwamba wengi ya wanandoa huko nchini humo wanashiriki zaidi mbinu na mipango ya uzazi pia kutokuwa na nafasi muafaka wa wanandoa au hata wapenzi kuonana kimwili, kuna laumiwa kwamba ndiko kulikosababisha idadi ya watoto wanaozaliwa kupungua mno.
Takwimu za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa zinaorodhesha Uhipania kama moja wapo ya mataifa yanayoongoza kwa kuporomoka kwa idadi ya watoto wanaozaliwa.
Nae waziri wa elimu hivi majuzi amewasilisha ripoti yake kwa serikali na baraza la mawaziri akilalamika kwamba madarasa ya shule hayana idadi ya kutosha ya watoto na akaonya kwamba hili huenda likaathiri Uhispania kiuchumi katika miaka ijayo.
Katika kushghulikia swala hilo kwa haraka waziri mkuu wa taifa hilo Mariano Rajoy amemteua Bi Edelmira Barreira kuwa waziri wa maswala ya ngono na mahaba
Kazi kubwa ya waziri huyo mpya ni kuja na mbinu za mikakati ya kuwahamasisha na kuuchochea umma wa Uhispania kurudi vitandani na kusaidia kutengeneza watoto ili kuijaza tena Uhispania.
Sign up here with your email